LIVE STREAM ADS

Header Ads

HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA YAZINDUA ZOEZI LA UTOAJI CHANJO YA POLIO KWA WATOTO

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Zaidi ya watoto 200,000 wenye umri kati ya miaka 0 hadi 10 katika halmashauti ya Jiji la Mwanza wanatarajiwa kupatiwa chanjo na matone ili kuwakinga na ugonjwa wa polio ambao vimelea vyake vimetajwa kubainika katika sampuli zilizopimwa mkoani Mwanza

Akizungumza katika uzinduzi wa zoezi la utoaji chanjo hiyo lililofanyika Jumanne Machi 24, 2026 katika Kituo cha Afya cha Mkolani jijini Mwanza, Afisa Tawala wa Wilaya ya Nyamagana, Magreth John amewahimiza wazazi na walezi kutoa ushirikiano kwa wataalam watakaopita katika maeneo yao kutoa chanjo hiyo.

"Chanjo hii tutaifanya pia kwa watoto waliokuwa wamepata chanjo ya polio hapo awali kwa sababu kuna viashria ambavyo vimeweza kuonekana ambavyo ya sasa itasaidia kuwakinga watoto" amesema Magreth na kuongeza;

"Zoezi hili ni letu sote hivyo pia viongozi wa Serikali za Mitaa mna wajibu kuhamasisha wananchi kupokea hii chanjo, lakini watoto wetu tuhakikishe kuanzia miaka 0 hadi 10w anapata chanjo". 
Akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu mkoani Mwanza, Mfamasia wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Gipson Simburya amesema tafiti zilizofanyika hivi karibuni zilibaini uwepo wa vimelea vya ugonjwa wa polio ambapo mtoto asipopatiwa chanjo husabisha kupooza viungo vya mwili na kusababisha ulemavu wa kudumu na wakati mwingine kupoteza maisha.

"Madhara anayoweza kupata mtoto mwenye vimelea vya polia ni kupooza, miguu inakuwa legelege na wakati mwingine kusababisha kifo" amesema Simburya.

Pia Simburya ameongeza kuwa "chanjo itatolewa kwa muda wa siku nne, tutapita mashuleni na nyumba kwa nyumba kuhakikisha watoto wote wanafikiwa, tuwaombe wazazi watoe ushirikiano ili kumkinga mtoto dhidi ya vimelea hivyo".

Akizungumza kwa niaba ya wananchi, diwani wa Kata ya Mkolani jijini Mwanza, John Mbira amesema jitihada za kuhamasisha wananchi kujishiriki zoezi hilo zimefanyika hatua ambayo anaamini itasaidia kuondoa imani potofu kwa baadhi ya wananachi ambao wamekuwa wazito kupokea chanzo za aina mbalimbali pindi zinapotangazwa kutolewa na Serikali.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI

No comments:

Powered by Blogger.