LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANANCHI NYAMAGANA WAPANDA MITI KUADHIMISHA SIKU YA MISITU DUNIANI 2026

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kushirikiana na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Nyamagana, imekabidhi miche elfu tano kwa wananchi wa Kata ya Lwanhima ili kupandwa katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuhifadhi mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Zoezi la kukabidhi miche hiyo limefanyika Alhamisi Machi 19, 2026 katika Mtaa wa Isebanda, likiambata na upandi miti katika Zahanati ya Isibanda na Shule ya Awali ya Nyabahigisi ambapo liliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi.

Hatua hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani ambayo kilele chake tarehe 21 Machi 2026 huku kauli mbiu ikiwa ni "Misitu ni Uchumi Endelevu, Tuhifadhi kwa Maendeleo ya Taifa".

Akizungumza katika zoezi hilo, Makilagi aliwahimiza wananchi kuitunza vyema miche hiyo ili kuleta manufaa ikiwemo matunda, kimvuli na kuhifadhi mazingira hatua itakayosaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Makilagi alisema Serikali inatumia gharama kuotesha miche hiyo na kuigawa bure kwa wananchi hivyo ni vyema kuhakikisha wanaitunza ili iwasaidie kuepuka gharama za kununua matunda, kupata kivuli na kupunguza hewa ya ukaa.

Naye Afisa Uhifadhi TFS Wilaya ya Nyamagana, Sharifa Kayonza alisema katika kuelekea kilele cha Siku ya Misitu Duniani, miche 9,765 imegawisha bure kwa wananchi ikiwemo ya matunda, urembo, matunda na kivuli

Wananchi wa Kata ya Lwanhima akiwemo Hassan Juma waliahidi kuitunza miti waliyokabidhiwa ili kupata manufaa mbalimbali ikiwemo matunda na hewa safi katika makazi yao.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi akiongoza zoezi la kupanda miche katika Kata ya Lwanhima.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi akiongoza zoezi la kupanda miche katika Kata ya Lwanhima.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi akikabidhi miche kwa wananchi
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi akikabidhi miche kwa wananchi
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi akikabidhi miche kwa wananchi
Viongozi na watumishi wa TFS wakishirikiana na wananchi kupanda miti katika Kata ya Lwanhima jijini Mwanza
Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani ni tarehe 21 Machi 2026 ambapo kaulimbiu ni "Misitu ni Uchumi Endelevu, Tuhifadhi kwa Maendeleo ya Taifa".

No comments:

Powered by Blogger.