TAMASHA LA PILI LA CHIFU HANGAYA KUFANYIKA MWANZA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Tamasha hilo litafanyika jijini Mwanza tarehe 19 na 20 mwaka huu 2026 katika uwanja vya Furahisha.
Kinachowavutia watu wengi ni matukio yanayotarajiwa kwenye tamasha hili linalofanyika kwa mara ya pili tangu liasisiwe mwaka jana.
Yaliyofanyika mwaka jana Machi 08, 2025 yaliwavutiwa watu wengi ambapo mwaka huu yameboreshwa zaidi.
Kuna waliovutiwa na mbio fupi za km 5 (Furahisha hadi mjini), mwaka huu pia zipo na hazina kiingilio, ni wewe na miguu yako na vifaa vya michezo basi.
"Wengine walipenda ngoma za makabila mbalimbali, mwaka huu nisiseme sana, maana kama wewe unachizika basi utachizika zaidi wiki ijayo, ngoma kama zote" amesema Mratibu wa tamasha hilo, Bernard James na kuongeza;
"Pia wanaopenda utani wa makabila, maonesho ya mavazi, michezo ya asili kama sarakasi, bao, mdako na mingine kibao sasa safari hii watakata kiu yao".
James amesisitiza kuwa wanaopenda chakula cha asili, kuonja ladha ya vyakula vya makabila kibao sasa wamefikiwa. Watakula vyakula na vinywaji halisi vya makabila mbalimbali.
Amesema burudani nyingi zitakuwepo uwanjani, za kila rika kutoka makabila mbalimbali mazuri yaliyo nchini.
Hakuna kiingilio kwenye tamasha hilo hivyo wananchi wanahimizwa kufika uwanja wa Furahisha kuufurahia, kuuenzi na kuurithisha utamaduni mzuri wa kitanzania kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

No comments: