LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANAVYUO MWANZA WAITIKIA JIPANGE TOUR

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Vijana kutoka vyuo mbalimbali jijini Mwanza ikiwemo SAUT, TIA, IFM, CBE, Mipango na Misungwi CDTTI, wamejitokeza kwa wingi kwenye mtoko wa Jipange University Tour ulioandaliwa na taasisi ya WBM Tanzania @wbm_tz

Lengo la mtoko huu ni kuhakikisha wanafunzi wanapata nafasi ya kushiriki kwenye jukwaa la Jipange ili kufahamu fursa mbalimbali zitakazowawezesha kujikwamua kiuchumi.
“Vinaja mnapaswa kutumia vizuri nguvu na muda kuijenga kesho yenu iliyo bora. Sisi CRDB tumewaletea huduma mbalimbali ikiwemo za mikopo ili kuwasaidia kutimiza ndoto zenu, ndiyo maana tunasema vijana Konekt na CRDB”- Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Stephen Adili akifungua Jipange University Tour jijini Mwanza.
“Tumelenga kuwazesha vijana wanaosoma vyuoni kuziona fursa ili kuondoa fikra za kuajiriwa baada ya kuhitimu. Tumewafikia vijana wa Dar es salaam, leo tuko Mwanza na tutaenda pia mikoa mingine”- Latifa Mohamed, Mkurugenzi taasisi ya WMB Tanzania, waandaaji wa Jipange University Tour.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi- Stephen Adili (katikati), Mkurugenzi WBM- Latifa Mohamed na Baraka Nyororo- Mkurugenzi Mwenza mgahawa wa Sato Sangara (kushoto).
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi kutoka Benki ya CRDB, Stephen Adili akikagua bidhaa za baadhi ya wanafunzi wajasiriamali walioshiriki tukio la Jipange University Tour jijini Mwanza.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi kutoka Benki ya CRDB, Stephen Adili (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
Wanavyuo mkoani Mwanza wakiwa kwenye jukwaa la Jipange University Tour.

No comments:

Powered by Blogger.