LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC MWANZA ATETA NA MADIWANI WA CHALINZE, MOSHI

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amewapokea madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze na Manispaa ya Moshi waliofika katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza ili kujifunza utekelezaji wa miradi ya kimkakati pamoja na ukusanyaji wa mapato.

Akizungumza na madiwani hao Jumatano Mei 2026, Mtanda alisema madiwani kufanya ziara za kimafunzo ni jitihada njema zinazoweza kusaidia Halmashauri zao kuanzisha na kusimamia vyato vya mapato.

Alisema uhai wa Halmashauri yoyote ile unategemea ukusanyaji wa mapato na ambayo haikusanyi mapato ni mufirisi na itakuwa na machungu kwani itashindwa kujiendesha na hata kuratibu ziara za kimafunzo.

"Halmashauri ikiwa na kipato kizuri, tusiishie kufanya ziara ndani ya nchi. Twende hata nje ya nchi kujifunza na kujenga mahusiano na miji mbalimbali. Mfano Chalinze madiwani watano wakienda China wanaweza kurudi wamejifunza kwamba kiwanda cha nanasi kinaweza kuleta mapato" alisema Mtanda.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Leon Lucas aliipongeza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa hatua kubwa ya uanzishaji na usimamizi wa miradi ya kimkakati ambayo imeongeza vyanzo vya ukusanyaji mapato.

Wakiwa jijini Mwanza, madiwani hao watajifunza na kutembelea miradi ya kimkakati ikiwemo daraja la Magufuli, stendi ya mabasi Nyegezi, soko kuu Mwanza na hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Leon Lucas.
Madiwani wa Halmashauri za Chalinze na Moshi wakiwa kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI

No comments:

Powered by Blogger.