UFUNGUZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA ROYAL (ROYAL ZONAL REFERRAL HOSPITAL) MWANZA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Fuatilia matangazo Mubashara #Live kutoka eneo la Ghana jijini Mwanza, kwenye hafla ya ufunguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Royal (Royal Zonal Referral Hospital).
Ni hospitali mpya, ya kisasa, yenye wataalam na vifaa tiba bora katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
KUHUSU UZINDUZI
Hospitali mpya ya Rufaa ya Kanda Royal iliyopo Ghana jijini Mwanza, imefunguliwa rasmi ikitarajiwa kutoa huduma bora za afya kwa wananchi hususani wakazi wa Kanda ya Ziwa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt. Lusako Mwaikasu amesema wamejipanga kuleta mapinduzi ya huduma bora za afya hospitalini hapo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dkt. Glory Simon amesema wamejipanga kutoa huduma kwa ufanisi mkubwa hivyo watanzania wategemee kunufaika na huduma bora za afya.
Mmoja wa wakazi wa Mwanza, Richard Nickson amesema wana Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla wamepokea kwa mikono miwili taarifa za ufunguzi wa Hospitali hiyo, wakitarajia huduma bora hasa za kibingwa.
Mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Hospitali ya Kanda Royal iliyopo Mtaa wa Ghana jijini Mwanza, anatarajiwa kuwa Rev. Dkt. Barnabas Mtokambali.

No comments: