WIZARA YA ARDHI YAWAHUDUMIA WANANCHI 1,400 DODOMA
Huduma hizo zilitolewa kufuatia maelekezo ya Mgeni Rasmi wakati wa kufunga Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2026, ambaye alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka.
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yalifanyika kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni 2026 katika Viwanja vya Chinangali Park, ambapo wakati wa kuyafunga, Mgeni Rasmi alielekeza Wizara ya Ardhi kuendelea kutoa huduma kwa wananchi hadi tarehe 30 Juni 2026 ili kuwapa wananchi wengi zaidi fursa ya kupata huduma za sekta ya ardhi.
Utekelezaji wa maelekezo hayo umewezesha wananchi wengi kupata huduma za ushauri, ufafanuzi wa masuala ya ardhi na huduma nyingine mbalimbali zinazotolewa na Wizara, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali za kusogeza huduma karibu na wananchi.

















No comments: