LIVE STREAM ADS

Header Ads

SHANGWE CHEM CHEM SAFARI LODGE WAKISHINDA TENA TUZO HOTEL BORA YA KIFAHARI AFRIKA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

  

Mussa Juma,Babati
mussasiwa@gmail.com 

Kwa mwaka wa pili mfululizo, hoteli ya kitalii ya Chem Chem Safari Lodge imeshinda tuzo ya hotel Bora ya kifahari barani Afrika katika tuzo ambazo ziliandaliwa na shirika la kimataifa la Utalii, World Travel Awards (WTA).

Chem Chem Safari Lodge  iliyopo eneo la hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori (WMA) la  Burunge, wilaya ya Babati,Mkoa wa Manyara imeshinda tuzo hiyo mfululizo mwaka 2025 na mwaka 2026.

Ushindi huu ni sehemu ya malengo ya muda mrefu ya waanzilishi wa hotel hiyo, Nicholas Negri na Fabia Bausch kuifanya Burunge WMA kuwa hifadhi ya Jamii Bora zaidi barani Afrika ,kwa kutoa huduma bora za Utalii,kuongezeka Wanyamapori na kuwa na mazingira bora zaidi ya kufanya Utalii wa kifahari.

Wakizungumzia baada ya kukabidhiwa tuzo hizo mbili, Lodge bora ya kifahari Tanzania na Afrika, wafanyakazi wa Chem Chem na viongozi wa Serikali Mkoa Manyara walisema mafanikio hayo ni mkakati wao wa Muda mrefu.

Meneja Mkuu wa Chem Chem Safari Lodge,Jorg Weytjens anasema ushindi huo unathibitisha huduma bora wanazotoa na kuvutia watalii.

"Tunashukuru Sana watalii kutoka sehemu mbalimbali Duniani kuendelea kutupigia kura na kutupa ushindi kutokana na huduma bora tunazotoa"anasema

Mkurugenzi wa halmashauri ya Babati vijijini,Anna Mbogo anasema ushindi wa Chemmchem unadhihirisha ushirikiano baina ya Serikali,wananchi wa vijiji 10 vinavyounda hifadhi hiyo na wafanyakazi wa Chemmchem.

"Sisi kama Serikali tunapongeza ushindi huu kwani utaendelea kutangaza wilaya yetu ya Babati lakini pia kuongeza mapato na kutimiza dhamira ya Rais Samia Suluhu kuvutia watalii Tanzania"amesema

Meneja Rasilimali watu wa Chem Chem  Jennifer Giray anasema ushindi waliopata unatokana na kuendelea kutoa huduma bora ambazo zinavutia watalii.

"Jambo kubwa tunashukuru Sana wakurugenzi wetu Nicolas na Fabia Kwa usimamizi mzuri, malengo makubwa waliotuwekea na sasa tunafanya vizuri Afrika"anasema 

Anasema wafanyakazi wa hotel hiyo wanafanyakazi Kwa ushirikiano mkubwa na katika mazingira Mazuri ambayo yanawavutia kutoa huduma bora 

Muongoza watalii wa Chem Chem Isack Joseph anasema wanajivunia tuzo hiyo na kuahidi wataendelea kutoa huduma bora zaidi Kwa watalii.

Joseph anasema wataendelea kutoa huduma Bora na kuvutia mamilion ya watalii na hivyo kuongeza mapato ya hotel na Kwa Serikali.

Meneja wa huduma katika hotel hiyo, George Andrew anasema lengo Lao wakati wote ni kutoa huduma bora Kwa watalii.

Hata hivyo alipongeza ushirikiano ambao wanapewa na Serikali kuanzia ngazi ya Taifa hadi vijijini na hivyo kuwafanya watalii kuwa Salama na wenye furaha wanapowatembelea Muda wote 

Ushindi wa Chem chem ulitangazwa katika hafla ya kutoa  tuzo hizo zilizofanyika wiki iliopita Zanzibar.

No comments:

Powered by Blogger.