LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAIFA GAS YAENDELEA KUFANIKISHA MKAKATI WA WATANZANIA WA KUTUMIA NISHATI SAFI

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

   

Balozi wa Matumizi ya Nishati Safi, Bi. Pilly Zubery, akijaribu pikipiki aliyokabidhiwa na Taifa Gas baada ya kufanikiwa kufikia na kuhamasisha zaidi ya kaya 50 kutumia nishati safi ya kupikia. Kulia ni Meneja Masoko wa Taifa Gas, Oscar Shelukindo, na kushoto ni Afisa Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Mary Lupamba.
Balozi wa Matumizi ya Nishati Safi, Bi. Pilly Zubery, akipokea kadi ya pikipiki kutoka kwa Meneja Masoko wa Taifa Gas, Oscar Shelukindo (kulia), huku kushoto akiwa Afisa Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Mary Lupamba, baada ya Pilly kufanikiwa kufikia zaidi ya kaya 50 katika kampeni ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Balozi wa Matumizi ya Nishati Safi, Bi. Pilly Zubery, akipokea kadi ya pikipiki kutoka kwa Meneja Masoko wa Taifa Gas, Oscar Shelukindo (kulia), huku kushoto akiwa Afisa Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Mary Lupamba, baada ya Pilly kufanikiwa kufikia zaidi ya kaya 50 katika kampeni ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Balozi wa Matumizi ya Nishati Safi, Bi. Pilly Zubery, akifurahia zawadi ya pikipiki aliyokabidhiwa na Taifa Gas baada ya kufanikiwa kufikia na kuhamasisha zaidi ya kaya 50 kutumia nishati safi ya kupikia.
Muonekano wa pikipiki iliyotolewa na Taifa Gas kama zawadi kwa Balozi wa Nishati, Bi. Pilly Zubery.
Meneja Masoko wa Taifa Gas Kanda ya Ziwa, Hawa Omary, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi ya pikipiki kwa Balozi wa Nishati, Bi. Pilly Zubery, baada ya kufanikiwa kufikia zaidi ya kaya 50 katika kampeni ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Afisa Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Mary Lupamba, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi ya pikipiki kwa Balozi wa Nishati, Bi. Pilly Zubery, baada ya kufanikiwa kufikia zaidi ya kaya 50 katika kampeni ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Meneja Masoko wa Taifa Gas, Oscar Shelukindo, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi ya pikipiki kwa Balozi wa Nishati, Bi. Pilly Zubery, baada ya kufanikiwa kufikia na kuhamasisha zaidi ya kaya 50 kutumia nishati safi ya kupikia.
Balozi wa Nishati Safi, Bi. Pilly Zubery, akizungumza baada ya kukabidhiwa zawadi ya pikipiki na Taifa Gas kwa kufanikiwa kufikia na kuhamasisha zaidi ya kaya 50 kutumia nishati safi ya kupikia.
Taifa Gas yaendelea kufanikisha mkakati wa watanzania wa kutumia nishati safi.

#Yatoa motisha ya pikipiki kupitia kampeni ya Balozi wa Nishati

Katika jitihada za kufanikisha mkakati wa serikali wa kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034, Kampuni ya Taifa Gas imeendelea kutoa elimu katika jamii nchini ambapo mwishoni mwa wiki imetoa zawadi ya pikipiki kwa Bi. Pilly Zubery mkazi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala kupitia kampeni yake ya Balozi wa Nishati iliyoanzishwa mwaka jana.

Kampeni ya Balozi wa nishati safi imelenga kuwawezesha na kuwahamasisha wananchi wa Msalala kutumia nishati safi ya gesi kwa ajili ya kupikia sambamba na kuwafanya mabalozi wa nishati hiyo katika maeneo yao na ilizinduliwa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambapo wananchi walipatiwa mafunzo ya nishati safi ya kupikia na mawakala 20 ambao ni mabalozi wa nishati kupatiwa mitungi 320 ya gesi kutoka kampuni ya Taifa Gas kwa ajili ya kusaidia katika uhamasishaji.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki hiyo Meneja Masoko wa kampuni ya Taifa Gas Oscar Shelukindo amesema kuwa kampeni ya Balozi wa Nishati imepata mafanikio makubwa ambapo wananchi wengi wa Msalala hivi sasa wameachana na matumizi ya mkaa na kuni zisizo salama kwa mazingira na kiafya na kuanza kutumia nishati safi ya gesi.

Ametoa pongezi kwa mshindi Bi. Pilly Zubery kwa kuwa mhamasishaji mzuri ambaye amekuwa wakala na balozi aliyeweza kufikisha elimu kwa kaya zaidi ya 50 na kuzibadilisha kutoka kwenye matumizi ya nishati zisizo salama na sasa zinatumia nishati safi na salama ya kupikia.

Shelukindo pia ametoa pongezi wa mabalozi wengine ambao wanaendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi na alishukuru mgodi wa Barrick Bulyanhulu ambao u,mekuwa mdau mkubwa katika kampeni na kutoa wito kwa wananchi wote wa Msalala kuhamia kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia ambayo ina gharama nafuu,inalinda mazingira na afya kwa watumiaji.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Taifa Gas Kanda ya Ziwa Hawa Omary amesema mwitikio wa matumizi ya nishati Halmashauri ya Msalala unazidi kuwa mkubwa ambapo kwa sasa wananchi wengi wameanza kutumia gesi tofauti na hali iliyokuwa hapo awali kabla ya kuanzishwa kwa kampeni hii. 

“Matokeo haya yanatia moyo na yanaonyesha dhamira ya Serikali kuhakikisha wananchi wanatumia nishati iliyo salama na yenye manufaa kwa afya na mazingira”,amesema.

Mwakilishi wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu katika hafla hiyo, Mary Lupamba ambayi ni Afisa Mahusiano ya jamii amesema Barrick itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali za kulinda mazingira na kushirikiana na wadau wengine wa kulinda mazingira na kuhamasisha matumizi ya nishati safi.

Naye mshindi wa zawadi ya pikipiki Pili Zubery amewashukuru waandaaji wa kampeni hii ya Balozi wa Nishati ambayo mbali na kuhamasisha nishati safi imeweza kuwa mkombozi wa wanawake ambao walikuwa wanatumia muda mwingi na nguvu kutafuta nishati ya kupikia pia imeweza kuwainua kiuchumi katika biashara zao ndogo ndogo.

“Wakati naanza biashara sikuwa na mtaji mkubwa lakini kutokana na mafunzo tuliyopatiwa na Taifa Gas kuhusu matumzi ya nishati safi niliweza kutembelea kaya nyingi na kutoa elimu niliyoipata na kuwezesha kaya zaidi ya 50 ku badilika kutoka kwenye matumizi ya nishati zisizo salama. 

“Nashukuru kwa kupewa zawadi ya pikipiki ambaye imekatiwa na bima ambayo nitaitumia katika kurahisisha biashara zangu katika usambazaji na kuwafikia wateja wengi zaidi”, amesema.

Serikali ilizindua Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia mnamo Mei 8, 2024, ikilenga kufikisha asilimia 80 ya wananchi wanatumia nishati safi ifikapo mwaka 2034, au hata asilimia 75 ifikapo 2030.Kampuni ya Taifa inazidi kuwa kinara wa kufanikisha mkakati huu ambapo inaendelea kupeleke elimu na huduma katika mikoa yote nchini.

Kampeni ya matumizi ya nishati safi kwa ajili ya kupikia ilianzishwa kitaifa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika juhudi za kuhakikisha watanzania hasa wanawake wanaondokana na matumizi ya mkaa na kuni kwa ajili ya kupikia.

No comments:

Powered by Blogger.