LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKUTANO MKUU WA ALAT TAIFA KUFANYIKA NOVEMBA 2026 MWANZA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
 Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), unatarajiwa kufanyika jijini Mwanza, ukijumuisha Halmashauri 184 na wajumbe mbalimbali wakiwemo Wakurugenzi, Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri nchini.

Mkutano huo ni moja ya mikutano ya kikanuni na unatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 500 ambapo utafanyika Novemba 14 hadi 16 mwaka huu 2026 jijini Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Sima Costantine amesema mkutano huo utakuwa na sehemu mbili ambapo mkutano wa kwanza utakuwa ni mkutano mkuu ambao utajadili mambo yatokanayo na Halmashauri.

"Mkutano wa pili utakuwa ni wa kazi ambao utazikutanisha taasisi mbalimbali zinazofanya kazi na Serikali za mitaa ambapo zitapata nafasi ya kuwasilisha mawasilisho na kutoa ajenda mbalimbali" amesema Sima

Sima amesema maandalizi ya mkutano huo tayari yameshaanza kufanyika huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoendelea kuruhusu na kutoa vibali vya kufanyika kwa mkutano huo.

Aidha ametoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza kuendelea kuwa wakarimu kwaajili ya kuwapokea wageni kwani ugeni huo ni mkubwa na utakuwa na fursa nzuri hususani katika kukuza uchumi.

Ameeleza kuwa Mkoa wa Mwanza unavivutio mbalimbali ikiwemo Hifadhi ya kisiwa cha Saa nane hivyo wanaendelea kuangalia namna nzuri ili wageni watakapofika waweze kutembelea vivutio hivyo.
Na Hellen Mtereko, Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.