HAKUNA BIASHARA ITAKAYOFUNGWA KWA SABABU YA KODI - CG MWENDA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda, amewahakikishia Walipakodi nchini kuwa hakuna biashara yoyote itakayofungwa kwa sababu ya kodi, akisisitiza kuwa TRA inalenga kuendelea kushirikiana na wafanyabiashara ili kuwawezesha kutekeleza wajibu wao wa kikodi na kuendeleza biashara zao.
Ameyasema hayo alipokutana na wafanyabiashara wa Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro Oktoba 19, 2026 alipowatembelea kwa lengo la kuwasikiliza na kutatua changamoto zao.
Amesema TRA itaendelea kusikiliza changamoto za wafanyabiashara na kuzitafutia ufumbuzi kwa kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kati ya Mamlaka hiyo na wafanyabiashara, huku akiwahimiza kutekeleza wajibu wao wa kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati.
Kamishna Mkuu Mwenda amesema TRA itaendelea kutoa elimu ya kodi kwa wananchi kwa nchi nzima ili kuwawezesha kujua haki zao katika masuala ya kodi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Dastan Kyoba, amesisitiza umuhimu wa wafanyabiashara kushirikiana na TRA na kufuata sheria na taratibu za kodi ili kukuza biashara zao na kuchangia maendeleo ya wilaya na taifa kwa ujumla.
Wafanyabiashara wa Wilaya ya Kilombero wameishukuru TRA kwa ziara ya Kamishna Mkuu, wakieleza kuwa kukutana naye kumewapa fursa ya kuwasilisha changamoto zao na kupata ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya kodi.








No comments: