LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAWAZIRI WAKUTANA MUHEZA KUTATUA MIGOGORO YA MASHAMBA YA UWEKEZAJI

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Leonard Akwilapo (wa pili kulia) akizungumza wakati wa kikao cha kujadili utatuzi wa migogoro ya mashamba ya uwekezaji katika wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga. Wa pili kushoto ni Waziri wa TAMISEMI Prof Riziki Shemdoe na kulia ni Naibu Waziri wa Mipango na Uwekezaji Dkt. Pius Chaya na Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Ayubu Sebabili.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Prof. Riziki Shemdoe (Wa pili kushoto) akizungumza katika kikao cha kujadili utatuzi wa migogoro ya mashamba ya uwekezaji katika wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga.



Naibu Waziri Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Dkt. Pius Chaya (Kulia) akisisitiza jambo wakati kikao cha kujadili utatuzi wa migogoro ya mashamba ya uwekezaji kwenye wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga. Katikati ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Leonard Akwilapo na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian. 


Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza Dkt. Jumaa Mhina akizungumza wakati wa kikao cha kujadili utatuzi wa migogoro ya mashamba ya uwekezaji katika wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga.







Baadhi ya wananchi walioguswa na mgogoro wa mashamba ya uwekezaji katika halmashauri ya Muheza mkoa wa Tanga wakielezea umiliki wao wa maeneo kwenye mashamba hayo mbele ya mawaziri wakati wa kikao cha kujadili utatuzi wa migogoro ya mashamba ya uwekezaji tarehe 18 Februari 2026. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

Na Munir Shemweta, WANMM Muheza.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Leonard Akwilapo, ameongoza kikao maalum cha mawaziri na wataalamu wa Serikali kujadili utatuzi wa migogoro ya mashamba ya uwekezaji katika Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga.

Kikao hicho kilifanyika Februari 18, 2026 katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Muheza, ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, aliyesisitiza umuhimu wa kutatua changamoto za ardhi zinazogusa wananchi na wawekezaji.

Katika kikao hicho, Dkt. Akwilapo aliambatana na Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe, pamoja na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Dkt. Pius Chaya. Viongozi hao walipata fursa ya kusikiliza maoni ya wananchi walioathiriwa na migogoro ya mashamba ya uwekezaji yaliyofutiwa umiliki mwaka 2016.

Mashamba yanayohusika katika mgogoro huo ni pamoja na Azimio/Kilapula Geiglitz, Bwembwera, Kibaranga, Kihuhwi, Lewa na Saguras, yote yaliyopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza. Wananchi waliowasilisha malalamiko yao waliomba Serikali kuhakikisha haki inapatikana, hususan kuhusu matumizi ya ardhi, fidia na umiliki halali.

Akizungumza baada ya kusikiliza pande zote, Waziri Akwilapo alisisitiza kuwa Serikali inalenga kuhakikisha migogoro ya ardhi inatatuliwa kwa haki, kwa kuzingatia sheria, maslahi ya wananchi na mazingira bora ya uwekezaji.

Alieleza kuwa maamuzi yatakayofikiwa yatasaidia kuimarisha utulivu wa kijamii, kuongeza uzalishaji na kuvutia uwekezaji endelevu katika sekta ya kilimo na maendeleo ya makazi.

Hatua hiyo ya Serikali imepokelewa kwa matumaini na wananchi wa Muheza, wengi wakiamini kuwa kikao hicho ni mwanzo wa suluhu ya kudumu ya migogoro ya ardhi iliyodumu kwa muda mrefu.

No comments:

Powered by Blogger.