LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAMPUNI YA SONGORO MARINE YAKABIDHI KIVUKO UGANDA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kampuni ya kizawa ya Songoro Marine iliyojikita katika ujenzi wa meli ndani na nje ya Tanzania imekamilisha ujenzi wa kivuko kikubwa kitakachokuwa na uwezo wa kubeba abiria 310.

Kampuni hiyo imekamilisha ujenzi wa kivuko hicho kitakachokuwa kinafanya safari zake kati ya Bukungu - Kagwara - Kaberamaido nchini Uganda.

Songoro marine ambayo imejikita na ujenzi wa vivuko, imeendelea kuaminiwa na serikali ya uganda katika ujenzi wa vivuko kadhaa nchini humo.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo, Meja Songoro akizungumza wakati wa kukabidhi kivuko hicho, amesema ujenzi wa kivuko hicho ulianza februari 2020 na kukabidhiwa Februari 20 mwaka huu. 

Kampuni ya Songoro Marine, ilisaini  mkataba wa ujenzi wa vivuko viwili pamoja na mashine ya kuondoa uchafu ziwani (dredger) kwa fedha za Uganda shilingi, 41,974,226,085.

Baada ya siku ya jana kampuni hiyo kukabidhi kivuko hicho kwa serikali ya Uganda, inaendelea na kivuko kingine kimoja ambacho kitakabidhiwa muda wowote.

No comments:

Powered by Blogger.