TAIFA GAS WAKUTANA NA WADAU KUWEKA MIKAKATI YA KUTOA HUDUMA BORA ZAIDI KWA WATEJA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mwenyekiti Mtendaji wa Taifa Gas, Hamis Ramadhan na Meneja Mkuu,Devis Deogratius wakikata utepe kuwakaribisha mawakala wakubwa (Super Dealers) wa kampuni kwenye kiwanda cha kutengeneza mitungi Kibaha.
Mwenyekiti Mtendaji wa Taifa Gas, Hamis Ramadhan akiongea na mawakala wakuu wa kampuni wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika kiwanda cha kutengeneza mitungi kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
Katika hafla hiyo mawakala walitunukiwa vyeti kwa kutambua mchango wao
Baadhi ya mawakala katika hafla hiyo
Baadhi ya mawakala katika picha ya pamoja na viongozi wa kampuni ya Taifa Gas
**
# Yafanya uwekezaji mkubwa kwa kujenga kiwanda cha mitungi , Pwani
Viongozi, wafanyakazi na mawakala wakuu wa kampuni ya kusambaza nishati bora ya gesi nchini ya Taifa Gas,wamekutana katika kiwanda kipya cha kutengeneza mitungi kilichopo Kibaha mkoani Pwani kwa ajili ya kuweka mikakati ya kuendelea kutoa huduma kwa wateja kwendana na kukua kwa biashara ya matumizi ya nishati safi ya gesi nchini sambamba na kupongezana kwa mafanikio yaliyopatikana kipindi kilichopita.
Akiongea kuhusiana na tukio hilo, Mwenyekiti Mtendaji wa Taifa Gas, Hamis Ramadhani amewapongeza wateja, mawakala wakuu wa kampuni, wafanyakazi na wadau wote kwa kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na kufanikisha kupata mafanikio yaliyopatikana hadi kufikia sasa.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa kampuni hiyo , Deogratias David amesema Taifa Gas itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha inatoa huduma bora zaidi kwa wateja ili kuzidi kupata mafanikio sambamba na kuhakikisha Tanzania inaendelea kua kinara katika maendeleo endelevu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia duniani.
“Dhamira ya Taifa gas ni kuunga mkono agenda ya nishati safi inayoongozwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuwarahisishia Watanzania maisha kutokana na matumizi ya nishati safi kwa ajili ya kupikia ili kuchochea ukuaji wa biashara zao na uchumi kwa ujumla sambamba na kulinda mazingira”, amesema Devis.
Amesema kuwa kampuni itaendelea kuwekeza ili kufanikisha mkakati wa kutoa huduma bora kwa wateja na kuwasogezea huduma kwa karibu katika maeneo yote nchini kupitia kwa mawakala wake wakuu.
Kwa upande wao mawakala wakuu wa kampuni hiyo wamepata fursa ya kutoa maoni yao kuhusiana na jinsi gani ya kufanikisha mkakati wa masoko wa kampuni ambapo pia walitoa pongezi kwa uongozi na wafanyakazi wa Taifa Gas kwa kuendesha shughuli zake kwa ubunifu na weledi kwa lengo la kuhakikisha watanzania wananufaika na matumizi ya nishati ya Gesi.
Mawakala hao pia wameweza kuona uwekezaji mkubwa uliofanywa na kampuni kwa kujenga kiwanda kipya na cha kisasa cha kutengeneza mitungi ya gesi ambacho ni moja ya utekelezaji wa kimkakati wa kampuni wa kuhakikisha mapinduzi ya kijana yanafanikiwa kwa watanzania wengi zaidi kwa kutumia nishati safi kwa ajili ya kupikia.
No comments: