BILIONI 35 KUINUA UPATIKANAJI WA MAJI MKINGA, MRADI WAFIKIA 65%
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com [18/03, 09:30] Okuly Blog: 

Zaidi ya wakazi 57,000 wilayani Mkinga mkoa wa Tanga wanatarajiwa kunufaika na mradi mkubwa wa maji wa Mkinga-Horohoro uliofikia asilimia 65 ya utekelezaji wake huku kijiji kimoja cha Mtimbwani kikiwa tayari kinapata huduma hiyo.
Mradi huo unatekelezwa na mkandarasi mzawa STC kwa gharama ya shilingi bilioni 35 ambapo utakapokamilika utaongeza huduma ya majisafi wilayani Mkinga kufikia asilimia 88.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa RUWASA mkoa wa Tanga Mha. Upendo Lugongo wakati akitoa taarifa ya mradi kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira iliyofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo Machi 17, 2026 ambapo alisema jumla ya vijiji 37 vinatarajiwa kunufaika baada ya mradi kukamilika.
Alisema katika awamu ya kwanza jumla ya vijiji 27 vitanufaika na tayari wakazi wa kijiji kimoja cha Mtimbwani wameshaanza kufurahia huduma ya maji ikiwemo shule na zahanati za kijiji hicho ambazo nazo zimeunganishiwa majisafi ya bomba.





No comments: