DC NYAMAGANA AANZA KUTATUA KERO ZA WANANCHI KATA KWA KATA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Mhe. Amina Makilagi ameagiza mitambo ya kukwangua na kushindilia barabara ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza kufika Kata ya Luchelele kufungua barabara zilizoharibiwa na mvua zilizonyesha hivi karibuni.
Mhe. Makilagi ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi katika Kata zote za Wilaya ya Nyamagana, iliyoanza Aprili 21, 2026 hadi Mei 19, 2026.
Katika ziara hiyo Kata ya Luchelele, Mhe. Makilagi pia ameahidi kwamba Serikali inaendelea kushughulikia changamoto zinazowakabili wananchi ikiwemo uhaba wa maji, umeme, ukosefu wa ujenzi wa ofisi za mitaa, migogoro ya rdhi pamoja na ujenzi wa shule katika maeneo yao.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Amina Makilagi akizungumza na wakati wa Kata ya Luchelele kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Mnangati katika Mtaa wa Malimbe.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI



No comments: