KONGAMANO LA WANAUME (MEN AT WORK) KUFANYIKA MWANZA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Men at Work ni jukwaa maalum linalowakutanisha wanaume kutoka maeneo mbalimbali kwa lengo la kujifunza, kujadili na kujengeana uwezo katika safari ya maisha.
Kupitia kongamano hili, washiriki hupata fursa ya kuimarika katika nyanja muhimu kama uchumi, ndoa na mahusiano pamoja na kukuza nidhamu binafsi na uwajibikaji katika nafasi zao kama wanaume ndani ya familia na jamii kwa ujumla.
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2015, Men at Work imeendelea kuwa chachu ya mabadiliko kwa wanaume wengi, ikiwa imefanikiwa kuandaa makongamano yenye tija ndani na nje ya Mwanza.
Athari yake imekuwa kubwa kiasi cha kuibua majukwaa mengine yenye mwelekeo sawa, ikiwemo "Kikao cha Wanaume", lakini chimbuko lake ni Men at Work.
Ushuhuda wa mafanikio na mabadiliko ya maisha ya washiriki ni mwingi na unaendelea kuongezeka kila mwaka na unatarajiwa kutolewa katika kongamano la wanaume jijini Mwanza.
Kongamano hilo la wanaume (Men at Work) linatarakiwa kufanyika jumamosi tarehe 26 Aprili 2026 katika ukumbi wa Chuo cha BOT, Capripoint jijini Mwanza kuanzia saa mbili asubuhi.
Mwandaaji wa kongamano hilo, Maxwell Chaila amesema jukwaa hilo ni linatoa fursa kwa wanaume kufahamiana na kujifunza safari ya mabadiliko chanya katika maisha yao.
Men at Work- Mwanaume Bora, Jamii Imara.

No comments: