WAKAZI WA MBUGANI JIJINI MWANZA WALIA NA UBOVU WA BARABARA, MAJI
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Wakazi wa Mtaa wa Mbugani A, Kata ya Mbugani katika Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, wameomba Serikali kuwasaidia kutatua kero ya ubovu wa barabara ya Mashiri SDA ili kuondokana na adha inayowakabili.
Wametoa ombi hilo Jumatatu Mei 11, 2026 kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi.
Mmoja wa wakazi hao, John Zacharia aliomba barabara hiyo kujemgwa kwa kiwango cha zege kutokana na kuwa kwenye mwinuko na kwamba wananchi wako tayari kujitolea nguvu kazi wakati wa ujenzi huo.
"Hii barabara inatutesa hata sisi bodaboda, akina mama wanalia migongo. Tunaomba utusaidie Mkuu wa Wilaya" alisema Werema Joseph huku akitoa angalizo barabara hiyo isijengwe kwa kutumia mawe bali zege.
Mbali na kuwasilisha kero hiyo, wananchi pia waliwasilisha kero ya kuchelewa kuunganishiwa huduma ya maji licha ya kulipia na kuomba DC Makilagi awasaidie.
Pia walimpongeza DC Makilagi kwa kuwasaidia kufikishiwa huduma ya umeme katika Mtaa wao baada ya kuwasilisha kero hiyo kwenye mkutano wa hadhara alioufanya miezi kadhaa iliyopita.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi alisema Mkandarasi kupitia TARURA amekabidhiwa kazi ya ujenzi barabara ya Mashiri SDA hivyo kazi inatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia wiki ijayo.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi akizungumza na wakazi wa Mtaa wa Mbugani A, Kata ya Mbugani jijini Mwanza ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kupokea na kutatua kero za wananchi Kata kwa Kata.
Afisa Tarafa ya Nyamagana, Danty Kombe akifafanua hoja mbalimbali kwenye mkutano huo.
Mkazi wa Mbugani jijini Mwanza, John Zacharia akiwasilisha hoja kuhusu kero ya barabara ya Mashiri SDA ili itafutuwe ufumbuzi.
Mmoja wa wakazi wa Mtaa wa Mbugani A, Florah John akiwasilisha kero ya changamoto ya maji ili kutafutiwa ufumbuzi wakati wa mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi.
Wananchi Mtaa wa Mbugani A, Kata ya Mbugani wakifuatilia mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi.
Wananchi Mtaa wa Mbugani A, Kata ya Mbugani wakifuatilia mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi.
Muonekano wa transifoma iliyofungwa Mtaa wa Mbugani A eneo la Mzambarauni, Kata ya Mbugani jijini Mwanza kutatua changamoto ya umeme iliyokuwepo hapo awali








No comments: