LIVE STREAM ADS

Header Ads

SERIKALI KUENDELEA KUPOKEA MAONI YA WANANCHI KUHUSU SHERIA YA NDOA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Zainab Katimba amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2026/2027, Serikali itaendelea na mchakato wa kukusanya maoni ya Wananchi kuhusu marekebisho ya Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, kifungu cha 13, ambacho kinaruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri wa miaka 15.

Naibu Waziri Katimba amesema hayo tarehe 13 Mei, 2026, Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi, Taska Restituta Mbogo ambapo amesema;

 "Sheria ya Ndoa wakati inatungwa mwaka 1971 ilianguliwa na ukusanyaji wa maoni kwa jamii kwa njia ya White Paper ambapo watanzania wote walishirikishwa. Aidha, tangu Sheria hii itungwe imeshafanyiwa marekebisho mara nne mwaka 1974,1980,1996 na mwaka 2006. Mheshimiwa mwenyekiti maoni yalikusanywa kwenye mikoa ya Dar es Salaam,Tanga, Mtwara, Lindi, Arusha, Dodoma na Mara kuhusu Sheria ya Ndoa Sura ya 29".

Aliendelea kusema "hata hivyo baada ya uchambuzi wa maoni yaliyokisanywa imeonekana kuna hitaji la kukusanya maoni zaidi katika mikoa iliyosalia zoezi ambalo limepangwa kuanza katika mwaka wa fedha 2026/2027 mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo Serikali itawasilisha Bungeni Muswada huo ambao utakua umezingatia maoni ya wananchi".

Katika hatua nyingine Naibu Waziri amelieleza Bunge kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kulinda Haki za Mtoto za Watoto wakiwemo Watoto wa kike ikihusisha ujenzi wa miundombinu ya elimu na upatikanaji wa elimu bila malipo.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Zainab Katimba.

No comments:

Powered by Blogger.