LIVE STREAM ADS

Header Ads

Jukwaa la uongozi, malezi la Dkt. Rasha Kelej kufungua fursa kwa mamilioni ya watu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kwa vijana wengi na viongozi wanaochipukia duniani, kupata mwongozo kutoka kwa viongozi wenye uzoefu ni moja ya changamoto kubwa zinazowakabili katika safari yao ya maendeleo binafsi na kitaaluma. 

Kutokana na hali hiyo wanaharakati na mtetezi wa haki za binadamu Dkt. Rasha Kelej amekuja na Jukwaa la Mtandao la Uongozi na Mlezi (Mentorship) ili kuleta mabadiliko makubwa kwa mamilioni ya watu wanaotafuta maarifa na hamasa ya kufikia ndoto zao.

Jukwaa hilo linaloitwa “Beyond Power; Leadership, Global Influence and Impact” limeanzishwa kwa lengo la kuwapa vijana, wanawake na watu wa kada mbalimbali fursa ya kujifunza misingi ya uongozi, ushawishi chanya katika jamii, maendeleo binafsi na namna ya kuleta mabadiliko yenye tija katika maisha ya watu wengine.

Kupitia jukwaa hilo, washiriki watanufaika na uzoefu wa zaidi ya miaka 32 wa Dkt. Kelej katika nyanja za uongozi, maendeleo ya jamii, elimu na uwezeshaji wa wanawake. Maarifa yatakayoshirikishwa yatawasaidia kujenga uwezo wa kujiamini, kufanya maamuzi sahihi, kuendeleza vipaji vyao na kuwa viongozi bora katika jamii zao.

Akizungumza kuhusu uzinduzi huo, Dkt. Kelej amesema kuwa lengo lake ni kuhakikisha maarifa na uzoefu wake vinawafikia watu wengi zaidi, hususan vijana na wanawake ambao wanahitaji mwongozo ili kufikia mafanikio.

“Maarifa na uzoefu vina thamani kubwa zaidi vinaposhirikishwa. Kupitia jukwaa hili, ninatarajia kuwahamasisha viongozi wa kesho kuamini uwezo wao, kuendeleza ujuzi wao na kuongoza kwa uadilifu, huruma na ujasiri,” alisema.

Wadau wa maendeleo wameeleza kuwa jukwaa hilo litakuwa na mchango mkubwa katika kukuza kizazi kipya cha viongozi wenye maono na uwezo wa kukabiliana na changamoto za kijamii, kiuchumi na kimazingira. 

Aidha, kwa kuwa linapatikana mtandaoni, watu kutoka maeneo mbalimbali duniani wataweza kufaidika bila kujali umbali au hali zao za kiuchumi.

Hatua hiyo inaongeza juhudi za Dkt. Kelej katika kuwekeza kwa watu kupitia elimu na ujenzi wa uwezo. Kupitia taasisi ya Merck Foundation, amesaidia maelfu ya wataalamu wa afya kupata ufadhili wa masomo na kuwapatia wasichana wengi barani Afrika fursa ya kuendelea na elimu yao.

Kwa maudhui yatakayokuwa yakisambazwa pia kupitia mitandao ya kijamii na majukwaa mengine ya kidijitali yanayofikia zaidi ya watu milioni tisa duniani, jukwaa hilo linatarajiwa kuwa chanzo muhimu cha maarifa, hamasa na mwongozo kwa watu wengi wanaotafuta mafanikio katika maisha na taaluma zao.

Uzinduzi wa jukwaa hilo unaonesha kuwa uwekezaji kwa watu, elimu na ushirikishwaji wa maarifa ni nguzo muhimu katika kujenga jamii bora na mustakabali wenye maendeleo endelevu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Na Mwandishi Wetu, UAE

No comments:

Powered by Blogger.