LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAAFISA MAENDELEO YA JAMII NI NGUZO MUHIMU YA MAENDELEO- KABUJE

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
rais wa Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (CODEPATA), Victor Kabuje, amesema Maafisa Maendeleo ya Jamii ni kiungo muhimu katika utekelezaji na usimamizi wa shughuli mbalimbali za maendeleo zinazogusa sekta zote za kijamii nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumatatu Juni 15, 2026 jijini Mwanza, Kabuje alisema wataalam hao wana jukumu kubwa la kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika miradi ya maendeleo, kuimarisha ustawi wa jamii na kulinda maadili pamoja na amani ya nchi.

Aidha, amewaomba waandishi wa habari kuwa mabalozi wa kuielimisha jamii kuhusu kazi zinazofanywa na Serikali kupitia Maafisa Maendeleo ya Jamii ili kuongeza uelewa na ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo.

Kabuje amesema Mkutano Mkuu wa CODEPATA unatarajiwa kufanyika Juni 17 hadi 19, 2026 jijini Mwanza, ambapo wataalam wa maendeleo ya jamii kutoka maeneo mbalimbali nchini watakutana kujadili mafanikio yaliyopatikana na kuweka mikakati ya chama hicho.
rais wa Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (CODEPATA), Victor Kabuje.
Viongozi wa CODEPATA wakiteta jambo na wanahabari jijini Mwanza wakati wa maandalizi ya Mkutano Mkuu wa chama hicho.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.