LIVE STREAM ADS

Header Ads

ZAIDI YA WAKAZI 12,000 KUNUFAIKA NA HUDUMA YA MAJI USAGARA- MWANZA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Zaidi ya wakazi 12,000 wa Kata ya Usagara mkoani Mwanza, wanatarajia kunufaika na mradi wa uboreshaji wa mfumo wa usambazaji maji, unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) kupitia ujenzi wa matenki ya maji na ulazaji wa mabomba makuu ya kusafirisha maji, ambao sasa umefikia asilimia 68 za utekelezaji.

Hayo yamebainishwa wakati wa kikao cha MWAUWASA na wananchi wanufaika wa Mtaa wa Nyang'homango wilayani Misungwi, kilichojadili kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo.

"Mradi huo unahusisha ujenzi wa tenki la maji la lita milioni 1 litakalopokea maji kutoka tenki jipya linalojengwa eneo la Kagera - Buhongwa la lita milioni 10, sambamba na ulazaji wa mabomba makuu ya kusafirisha maji kwa urefu wa km 10.5" amefafanua Mhandisi Nuhu Said, Msimamizi wa Miradi MWAUWASA.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi, Mwenyekiti wa Mtaa huo, Anthon Kalongo amepongeza jitihada endelevu za Serikali kupitia Wizara ya Maji na MWAUWASA kwa kudhamiria kuendelea kuwafikishia wananchi huduma hiyo muhimu katika maeneo mbalimbali, na kwamba hatua hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa kuboresha maisha ya watu na kuchochea maendeleo.

No comments:

Powered by Blogger.