WMA YAUNGANA NA WATANZANIA KUWAENZI MASHAUJAA WA TAIFA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Wakala wa Vipimo (WMA) wameshiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa iliyofanyika katika Viwanja vya Mnara wa Mashujaa, Mtumba, jijini Dodoma, ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Maadhimisho hayo yaliyofanyika Julai 25,2026 yamewakutanisha viongozi wa Serikali, taasisi mbalimbali za umma na binafsi, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi kwa lengo la kuwakumbuka na kuwaenzi mashujaa waliojitolea kwa ajili amani na maendeleo ya Taifa.
Wakala wa Vipimo (WMA) imewakilishwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Bw. Alban M. Kihulla, na baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Vipimo kutoka Ofisi ya Mkoa wa Dodoma.
WMA inaungana na Watanzania wote katika kuwaenzi mashujaa wa Taifa waliotoa mchango mkubwa kwa ajili ya amani na maendeleo ya nchi, huku ikiendelea kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia misingi ya uwajibikaji na utumishi wa umma.




No comments: