MATOKEO CHANYA YA MRADI WA ELIMU WA BARRICK-TWIGA FUTURE FOWARD EDUCATION PROGRAM YAANZA KUONEKANA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Muonekano wa bweni la kisasa lililojengwa kupitia mradi wa elimu wa Barrick -Twiga
Muonekano wa sehemu ya madarasa ya kisasa yaliyojengwa kwa fedha kutoka Barrick
Muonekano wa sehemu ya madarasa ya kisasa yaliyojengwa kwa fedha kutoka Barrick
Viongozi wa CCM na Serikali na madiwani mkoani Njombe wakibadilishana mawazo baada ya kufanya ziara ya kikazi katika sekondari ya Ulayasi mkoani Njombe
Viongozi wa CCM na Serikali na madiwani mkoani Njombe wakibadilishana mawazo baada ya kufanya ziara ya kikazi katika sekondari ya Ulayasi mkoani Njombe
Wakikagua moja ya bweni lililojengwa kupitia mradi wa elimu wa Barrick-Twiga
Muonekano wa miundombinu ya bweni jipya lililojengwa kupitia mradi wa elimu wa Barrick -Twiga
Viongozi wakitembelea miundombinu ya vyoo vinavyoendelea kujengwa
Muonekano wa Madarasa ya zamani katika shule hiyo
Mradi wa kusongesha mustakabali wa elimu mbele ujulikanao kama Barrick-Twiga Future Foward Education Program unaotekelezwa na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick unazidi kuleta athari chanya kwenye shule za sekondari ulipotekelezwa nchini kote kutokana na kuwezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora ya kupata elimu na kufanikisha kuongeza idadi ya ufaulu wa wanafunzi.
Shule kongwe ya sekondari Ulayasi iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe ni miongoni mwa shule ambayo hapo awali ilikuwa inakabiliwa na miundombinu ya madarasa, mabweni na vyoo na baada ya kufikiwa na mradi huu sasa kero hizo zimeondoka na wanafunzi wanasoma katika mazingira bora yanayotakiwa kwa kupata elimu.
Akiwasilisha taarifa kwa viongozi wa mkoa wa Njombe waliofanya ziara ya kikazi shuleni hapo, Mwalimu Hamika Mgaya ambaye ni Mkuu wa shule alisema mradi wa Barrick-Twiga umebadilisha mazingira ya shule hiyo kuwa bora kupitia uwezeshaji wa shilingi milioni 597 ambazo zimefanikisha ujenzi wa mabweni matatu ya kisasa,vyumba 7 vya madarasa na matundu 16 ya vyoo.
Mwalimu Hangaya alisema fedha zilizotolewa na Barrick zimewezesha kuondoa changamoto ya upungufu wa mabweni,vyoo na madarasa na kuleta tumaini jipya la wanafunzi kufanya vizuri zaidi kitaaluma kutokana na kusomea katika mazingira rafiki ambayo pia yamepunguza matukio ya utoro wa wanafunzi.
Akitoa ushuhuda kwa niaba ya wanafunzi wenzake kuhusiana na athari chanya za mradi huu, Jackline Dismas Likata amesema kabla ya mradi huo kulikuwepo na mrundikano wa wanafunzi madarasani,kwenye mabweni na upungufu wa mashimo ya vyoo lakini kwa sasa changamoto hizo zimeondoka wanasoma katika mazingira rafiki yanayowawezesha kuwafanya vizuri katika masomo yao.
Naye Mwanafunzi Ipyana Mwanigule alitoa shukrani kwa Serikali na kampuni ya Barrick kwa kufanikisha ujenzi huo ambao umewezesha uwepo na mazingira rafiki ya kusoma hapo shuleni pia kuondoa kero za magonjwa ya mara kwa mara kwa wanafunzi ambayo yalisababishwa ma msongamano wa wanafunzi na matumizi ya vyoo visivyotosha na vilivyokuwa kwenye hali mbaya.
"Kwa sasa madarasa yetu yana umeme tunaweza kujisomea mpaka usiku bila tatizo pia maji yanatoka wakati wote hali inayosabisha vyoo tunavyotumia kuwa safi",alisema.
Akiongea kwa niaba ya viongozi wenzake baada ya kutembelea miundombinu ya shule hiyo katibu wa siasa na uenezi CCM Mkoa wa Njombe Josaya Luoga alitoa rai kwa wanafunzi na walimu kuitumia vizuri miundombinu hiyo mipya na kuitunza ili iweze kunufaisha vizazi vingine huku Mwenyekiti wa UWT Mkoa Dk. Scholastica Kevela, akisisitiza suala la maadili kwa wanafunzi wanaosoma shuleni hapo.
Naye Diwani wa Kata ya Mlangali, Amos Basili Mtweve ameipongeza Barrick kwa kuendelea kufadhili miradi ya elimu nchini na kuongeza kuwa mradi huo utakapokamilika kabisa utapaisha zaidi kiwango cha ufaulu wa wanafunzi.
Mradi wa Barrick-Twiga Future Forward Education ambao kwa sasa umeingia katika awamu ya pili unatekelezwa kwa fedha kiasi cha shilingi bilioni 70.5 zilizotolewa na kampuni ya Barrick Mining Corporation ambayo kwa hapa nchini inaendesha shughuli zake kwa ubia na serikali kupitia kampuni ya Twiga .
Malengo makuu ya program hii ni kufanikisha kuongeza na kuboresha miundombinu ya shule za sekondari za serikali za elimu ya juu (Advanced Level) ili kuongeza idadi ya wanafunzi wanaochaguliwa ambao walikuwa wanakosa fursa ya kuendelea na masomo kutokana na uhaba wa miundombinu sambamba na kuhakikisha wanapata elimu katika mazingira rafiki ukiwa unalenga kufanikisha ujenzi wa madarasa 1,090,majengo ya maliwato na vyoo 1,660 na mabweni 270 katika shule 161 nchini kote.
Katika awamu ya kwanza ya mradi umefanikisha ujenzi wa vyumba vya madarasa ya kisasa 374,mabweni ya kisasa 89 na vyoo 569.









No comments: