BARAZA LA UWEZESHAJI KIUCHUMI LIWAFIKIE WANANCHI – PROF KABUDI
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na wenye Ulemavu Prof. Palamagamba Kabudi amelitaka Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi (NEEC) kuhakikisha kwamba Baraza linawafikia na kuwagusa wananchi na kwamba kupitia Baraza wananchi wafahamu kuhusu mifuko na programu zote za uwezeshaji wananchi, fursa zinazotolewa na namna wanavyoweza kuzipaga fursa hizo.
Prof. Kabudi ameyasema hayo alipokutana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi Bw. Jabiri Makame.
Prof. Kabudi pia alimpongeza Bw. Jabiri Makame kwa kuteuliwa na kumshukuru Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wa kumteua na kwamba uzoefu alioupata katika nafasi ya Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa utasaidia kufikia malengo ya NEEC.
Kwa upande wake Bw. Jabiri Makame, alimshukuru Mhe. Prof Kabudi kwa maelekezo yake na kuahidi kwenda kuyafanyia kazi maelezo hayo kwa kushirikiana na watumishi wenzake ili kukidhi matarajio ya wananchi hasa katika wakati huu ambao Taifa letu limeanza kutekeleza Dira ya Taifa 2050.


















No comments: