WMA YASHIRIKI UZINDUZI WA MAJENGO YA SERIKALI NA BARABARA ZA LAMI MTUMBA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Na Robertha Makinda WMA - Dodoma
📍30 Oktoba, 2026
Wakala wa Vipimo (WMA) imeshiriki katika hafla ya uzinduzi wa majengo ya ofisi za Wizara na Taasisi za Serikali pamoja na barabara za lami katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, iliyofanyika leo, Oktoba 30, 2026.
Hafla hiyo ni kielelezo cha hatua kubwa zinazofanywa na Serikali katika kuboresha miundombinu, kuimarisha utendaji wa taasisi za umma na kuweka mazingira bora ya utoaji wa huduma kwa wananchi.
Wakala wa Vipimo (WMA) inatoa pongezi na shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi wake mahiri, wenye dira, maono na dhamira ya dhati ya kuwaletea Watanzania maendeleo.
Chini ya uongozi wake, Tanzania imeendelea kushuhudia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayogusa maisha ya wananchi.
Ujenzi na uzinduzi wa majengo haya ya kisasa ya ofisi za Wizara na Taasisi za Serikali pamoja na barabara za lami katika Mji wa Serikali Mtumba ni miongoni mwa matokeo ya uongozi bora wa Rais Samia.
Taifa.





















No comments: