TANZANIA YAPONGEZWA KUUNDA TUME YA KUCHUNGUZA MATUKIO YA UCHAGUZI MKUU 2025
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Tanzania imepongezwa na Kamishna wa Baraza la Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk kwa kuunda Tume ya kuchunguza matukio ya Uchaguzi Mkuu 2025.
Turk alitoa pongezi hizo wakati akitoa taarifa inayoangazia maeneo yaliyokumbwa na changamoto ya vita na migogoro duniani katika kikao cha 61 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kilichofanyika Geneva, Uswisi.
Akizungumza katika kikao hicho,
Kamishna Turk alisema hatua iliyochukuliwa na Tanzania kuanzisha Tume ya kuchunguza kilichojiri Oktoba 29, ni hatua muhimu inayojali haki za binadamu.
Tume ya kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea Oktoba 2025 ilianza rasmi majukumu yake Desemba 2025, kwa mujibu wa Sheria ya Tume za Uchunguzi, Sura ya 32, ikiundwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.


No comments: