MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WATAKIWA KUCHOCHEA MAENDELEO KWA WANANCHI
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Maafisa Maendeleo ya Jamii nchini wametakiwa kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo huku wakiwasaidia kutambua fursa zinazopatikana katika maeneo yao.
Rai hiyo inetolewa Ijumaa Juni 19, 2026 jijini Mwanza na Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum- Eliakim Maswi
wakati akifunga kongamano la 18 la Chama cha Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (CODEPATA)
Maswi alisema Maafisa Maendeleo ya Jamii wanatakiwa kufanya kazi kwa weledi huku wkiwajibika katika kuhakikisha wanajenga jamii bora yenye mtazamo na mawazo chanya.
Aliongeza kuwa Taifa lenye uchumi imara linajengwa na watu wenye maadili, ubunifu na uzalendo ambapo kada ya maendeleo ya jamii ina mchango mkubwa katika kuzalisha mawazo mapya yenye kuleta usuhishi wa changamoto za wananchi na hivyo kufikia mafanikio ya Dira 2050.
Naye Raisi wa CODEPATA, Victor Kabuje aliomba Srikali kuendelea kuboresha kada ya Maafisa Maendeleo ya Jamii ambao ni chachu ya maendeleo kwa wananchi na Taifa katika Dira ya 2030.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum- Eliakim Maswi.
Rais wa CODEPATA, Victor Kabuje.
Katibu Tawala Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Thomas Salala akitoa salamu kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Elikana Balandya.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum- Eliakim Maswi (kushoto) akikabidhi cheti cha pongezi kwa Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Misungwi (Misungwi CDTTI), Arch. Charles Achuodho (kulia) kwa kuwa miongoni mwa wadau waliofanikisha Mkutano wa CODEPATA.

Viongozi mbalimbali wakiwa na mgeni rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum- Eliakim Maswi.
Maafisa Maendeleo ya Jamii wakiwa kwenye hitimisho la Mkutano Mkuu wa CODEPATA 2026 jijini Mwanza.
Maafisa Maendeleo ya Jamii wakiwa kwenye hitimisho la Mkutano Mkuu wa CODEPATA 2026 jijini Mwanza.

No comments: