LIVE STREAM ADS

Header Ads

SEMA NA WAZIRI KUZINDULIWA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Wizara ya Katiba na Sheria ipo katika hatua za mwisho za kuzindua siku maalum itakayowapa wananchi fursa ya kuzungumza moja kwa moja na Waziri ili kuwasilisha na kupata ufumbuzi wa changamoto zao za kisheria.

Kwa mujibu wa taatifa ya Wizara imesema kuwa hatua hiyo ni jitihada ya Serikali ya kuwafikia wananchi wenye changamoto mbalimbali za kisheria na kuwapatia msaada kwa wakati.

Uzinduzi wa siku hiyo maalum unatarajiwa kufanyika tarehe 17 Machi 2026, ambapo Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Juma Homera, atazindua rasmi utaratibu huo kupitia kituo cha huduma kwa mteja cha Wizara

Imeelezwa kuwa kupitia utaratibu huo wananchi watapata fursa ya kupiga simu katika kituo hicho kupitia namba 0262160360 au 0800004004, ambapo simu zao zitapokelewa moja kwa moja na Waziri wa Katiba na Sheria ili kusikiliza changamoto zao na kuzitolea ufumbuzi.

Mpango huo unalenga kuimarisha mawasiliano kati ya Serikali na wananchi, pamoja na kurahisisha upatikanaji wa huduma na ushauri wa kisheria kwa wananchi.

No comments:

Powered by Blogger.