LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Sangu ashiriki shughuli za uvuvi Kirumba Mwanza, katika mwendelezo wa utoaji elimu ya Skimu ya Hifadhi ya Jamii

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu akijionea shughuli za uvuvi katika maeneo ya kazi ya wavuvi katika Soko la Kimataifa la Samaki Kirumba jijini Mwanza.

Mhe. Sangu pia ameshiriki kuvua samaki akishirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba.

Hatua hiyo ni mwendelezo wa utoaji elimu kwa makundi mbalimbali kuhusu Skimu ya Hifadhi ya mafao kupitia mfuko wa NSSF.

No comments:

Powered by Blogger.