WAJUMBE WA BODI SHIRIKA LA TEENS CORRIDOR WAPEWA MAFUNZO
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Shirika la vijana la Teens Corridor (Teens Corridor Organization- TCO) la jijini Mwanza, limetoa mafunzo kwa wajumbe wake wa bodi ili kuwajengea uwezo kutimiza majukumu yake kwa weledi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Sophia Nshushi amesema mafunzo hayo yamewezesha Wajumbe wa Bodi ya Shirika hilo kufahamu wajibu na majukumu yao pamoja na Sera mbalimbali.
Nshushi amesema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Vijana Plus unaotekelezwa na mashirika 40 nchini kupitia ufadhili wa Shirika la Save The Chilren na Umoja wa Ulaya kwa lengo la kuimarisha utendaji kazi wa mashirika yanayoongozwa na vijana.
Mmoja wa Wajumbe wa Bodi ya Shirika hilo, Lilian Rubuga amesema mafunzo hayo yataimarisha utendaji kazi na mahusiano baina yao na wafanyakazi huku wakifahamu pia mipaka ya utendaji kazi hatua itakayosaidia ukuaji wa taasisi.
Kwa upande wake Mkufunzi wa mafunzo hayo, Hasna Ally amesema Wajumbe wa Bodi wakitambua wajibu na majukumu yao, kushirikiana na uongozi na kufahamu Sera za Shirika, watasaidia Shirika ukuaji na kufikia malengo ya shirika.
Mafunzo hayo yamefanyika siku mbili yakiambatana na uwasilishaji wa ripoti ya utendaji kazi wa shirika katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka huu 2026 ambapo wajumbe wa bodi walipata fursa ya kujadili ripoti hiyo.
Na George Binagi, Mwanza
Mwezeshaji wa mafunzo kwa Wajumbe wa Bodi ya Shirika la vijana la Teens Corridor la jijini Mwanza akiwasilisha mada.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Teens Corridor, Sophia Nshushi akiwasilisha mambo ya msingi ambayo Bodi inapaswa kuzingatia ili kutekeleza vyema majukumu yake.
Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Teens Corridor, Lilian Rubuga akiwasilisha mikakati baada ya majadiliano.
Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Teens Corridor wakijadili ripoti ya shirika hilo katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka.
Wafanyakazi wa Shirika la Teens Corridor wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Wafanyakazi wa Shirika la Teens Corridor wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Wafanyakazi, wajumbe wa bodi ya Shirika la Teens Corridor na Mkufunzi wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Wafanyakazi, wajumbe wa bodi ya Shirika la Teens Corridor na Mkufunzi wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Teens Corridor (Teens Corridor Organization- TCO), Sophia Nshushi.
Tazama Video hapa chini
PIA>>> BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI










No comments: