DUNIA YAIPONGEZA TANZANIA: UNODC YAIWEZESHA DCEA KWA TEKNOLOJIA MPYA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imepokea vifaa vya kisasa vya uchunguzi wa kimaabara kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC), ikiwa ni pongezi baada ya kutambua mafanikio yaliyofikiwa na Tanzania katika udhibiti wa dawa za kulevya nchini.
Pongezi hizo zimetolewa tarehe 22 Aprili 2026 jijini Dar es Salaam na ujumbe wa UNODC ukiongozwa na Mwakilishi wa Kanda ya Afrika Mashariki, Ali El-Bereir, ambaye aliipongeza Tanzania kwa jitihada zinazofanyika katika kudhibiti biashara na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na kemikali bashirifu.
Vifaa hivyo hutokewa mahsusi kuzijengea uwezo taasisi zinazosimamia udhibiti wa dawa za kulevya katika ngazi ya kimataifa chini ya mpango wa Kimataifa wa Port Security and Safety of Navigation Programme (EU PSP). huo umetolewa chini ya mpango wa kimataifa wa Port Security and Safety of Navigation Programme (EU PSP).
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na mashine za kisasa zenye uwezo wa kubaini kwa haraka aina mbalimbali za dawa za kulevya na kemikali zinazodhibitiwa hata zikiwa ndani ya vifungashio vyake bila kufunguliwa. Hivyo, kuwezesha ufanisi wa kichunguzi na kuboresha utendaji kazi wa Mamlaka.
Aidha, UNODC imeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania kwa kutoa mafunzo na kuwajengea uwezo maafisa wa DCEA ili kuimarisha mapambano.





















No comments: