LIVE STREAM ADS

Header Ads

WADAU WA MAZINGIRA WATAHADHARISHA UCHAFUZI WA ZIWA VICTORIA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Wadau wa mazingira jijini Mwanza wametahadharisha kwamba hatari ya uchafuzi wa wa mazingira hasa ziwa Victoria, bado inaendelea kuonekana kutokana na ziwa hilo kusheheni taka mbalimbali hususani za plastiki.

Hayo yamebainishwa Jumamosi Aprili 18, 2025 na Mratibu Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Synergistic Globe, Angelina Tabu Manyama wakati wa zoezi la kufanya usafi katika fukwe za Ziwa Victoria ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa Watoto Marafiki wa Mazingira (Plastic changeMakers) katika Ziwa Victoria.

"Mradi huu mdogo ambao pia upo chini ya ufadhili wa Shirika la Global Greengrants Fund (GGF), unalenga kuwaandaa watoto kuwa mabalozi wa mazingira hususani katika kudhibiti taka za plastiki Ziwa Victoria" alisema Manyama.

Alisema kupitia zoezi la kufanya usafi katika kwenye fukwe za Ziwa Victoria, pia watoto wanaelimishwa kuhusu madhara ya plastiki zikiingia ziwani na badala yake wafahamu umuhimu wake kama malighafi katika kutengeneza vitu mbalimbali ikiwemo mapambo ya nyumbani na ofisini.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Vitus Medard alisema zoezi la kuwaelimisha watoto kutunza Ziwa Victoria ni endelevu, lengo likiwa ni kuhakikisha wanakuwa mabalozi wa mazingira kuanzia umri mdogo.

Nao baadhi ya watoto wakiwemo Justina Stephano na Japhet Patrick walioshiriki zoezi la kufanya usafi na kuokota chupa za plastiki katika ufukwe wa Ziwa Victoria uliopo Luchelele walisema walisema wao ni marafiki wa Ziwa Victoria hivyo wasingependa kuona Ziwa hilo linachafuliwa hasa kwa taka za plastiki baada ya matumizi ya vinywaji kama maji na soda.

Shirika la Synergistic Globe kupitia mradi wa Marafiki wa Ziwa Victoria tayari limeandaa mtaala maalumu wa kufundisha watoto madhara ya plastiki ulio katika maandishi na pia kwenye mfumo wa picha mjongeo (video za cartoon), ili kuhakikisha mabalozi wa mazingira wanapatikana katika umri mdogo.
Mratibu Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Synergistic Globe, Angelina Tabu Manyama.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Vitus Medard.
Mtoto rafiki wa Ziwa Victoria, Justina Stephano.
Mtoto rafiki wa Ziwa Victoria, Japhet Patrick
Watoto marafiki wa Ziwa Victoria wakifanya usafi na kuondoa taka za plastiki na kisha kuzitumia kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo mapambo.
Watoto marafiki wa mazingira wakifundishwa jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali kwa kutumia taka za plastiki kama jitihada za kupunguza hatari ya taka hizo kuzagaa ovyo na kuingia ziwani.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI

No comments:

Powered by Blogger.