CHUO CHA MISUNGWI CDTTI CHAWANOA VIJANA KULINDA MUUNGANO WA TANGANYIKA, ZANZIBAR
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Misungwi (Misungwi CDTTI) kilichopo mkoani Mwanza, kimeandaa na kuendesha mdahalo wa Maadili na Uzalendo kwa wanafunzi wa chuo hicho, ili kuwajengea ari ya kuenzi na kuulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mdahalo huo umefanyika Ijumaa Aprili 24, 2026 chuoni hapo ukihudhuriwa na wanafunzi, watumishi wa chuo na viongozi wa dini huku mgeni rasmi akiwa Katibu Tawala Wilaya ya Misungwi, Abdi Makange.
Mkuu wa Chuo cha Misungwi CDTTI, Arch. Charles Achuodho akitoa neno la ufunguzi wakati wa ufunguzi wa mdahalo huo.
Katibu Tawala Wilaya ya Misungwi, Abdi Makange akihitimisha mdahalo huo.
Wanafunzi Chuo cha Misungwi CDTTI wakifuatilia mdahalo wa Maadili na Uzalendo.
Maadili na Uzalendo ni msingi wa kuendelea kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliosaidia kuzaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Aprili 26, 1964.
Hayo yamesisitizwa kwenye mdahalo ulioandaliwa na Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Misungwi (Misungwi CDTTI) Mwanza, kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 62 ya Muungano mwaka huu 2026.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI












No comments: