LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANANCHI SHINYANGA WAALIKWA KUPATA MSAADA WA KISHERIA BURE

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, amewataka wananchi wa mkoa huo kujitokeza kupata huduma za msaada wa kisheria zitakazoanza kutolewa kuanzia tarehe 6 hadi 20 Mei 2026, kwa muda wa siku kumi na tano katika halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga.

Mhe. Mhita ametoa wito huo Jumanne tarehe 5 Mei 2026 akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Mkuu wa Mkoa Shinyanga, akisisitiza kuwa huduma hizo zinatolewa bila malipo yoyote kwa wananchi wote kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Awamu ya Pili.

Utoaji wa huduma za Msaada wa Kisheria utafanyika katika Halmashauri zote sita za mkoa ikuhusisha Kata, Vijiji na Mitaa yote iliyopo.

No comments:

Powered by Blogger.