LIVE STREAM ADS

Header Ads

WATEJA WAPYA 1500 WAENDELEA KUUNGANISHIWA MAJI MWANZA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Agizo la Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kwa watendaji wa Wizara hiyo la kuwaunganishia huduma ya maji safi wananchi limeendelea kutekelezwa.

Aweso alitoa agizo hilo Juni 17 mwaka huu la kuhakikisha wananchi walioomba na kulipia kuunganishwa na huduma ya maji wanaunganishiwa mara moja.

Watendaji wa Wizara hiyo wakiongozwa Kaimu Mkurugenzi wa Mwauwasa, Mhandisi Charles Mafie na Kaimu Mkurugenzi msaidizi wa usanifu na utekelezaji wa miradi, Mhandisi Leonard Msenyele, wametekeleza agizo hilo katika maeneo mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya hatua za kuunganishia wananchi huduma hiyo, Mhandisi Mafie, amesema mpaka sasa wateja zaidi ya 50 wameunganishwa na huduma ya maji safi na kazi hiyo inaendelea.

Amesema wanaendelea na zoezi la kuunganishia wateja huduma hiyo mpaka na kuhakikisha huduma ya maji inaimarika.

Mafie amesema Mamlaka ya Maji Mwauwasa, ilikuwa na wateja 1500 waliokuwa wameomba na kulipia gharama za kuunganishiwa maji na sasa wanaendelea na mchakato.

Amesema, serikali itahakikisha hatua zote zinatekelezwa kwa wananchi wote wanaomba huduma hiyo wanatekelezewa haki yao ya msingi.

Mafie anafafanua kuwa, kulikuwa na changamoto mbalimbali zilichangia wananchi hao kuchelewa kuunganishiwa huduma ya maji na sasa zimetatuliwa.

Anaendelea kueleza kuwa, mteja anapofanya maombi na kulipia fedha, anapaswa kuunganishiwa maji ndani ya siku saba tangu alipoomba.

Baadhi ya wakazi wa Isamilo genge la Washashi na Buhongwa ambao wameunganishiwa huduma ya maji safi wameipongeza serikali kwa kuchua hatua za haraka kupata huduma.

Wamesema wanampongeza Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kwa utendaji wake wa kazi ambaye amehakikisha wameunganishiwa huduma ya maji safi na salama.

Mamlaka ya majisafi na usafi wa Mazingira jijini Mwanza - Mwauwasa inahudumia zaidi ya asilimia 87 ya wakazi wa Jiji hilo. Upatikanaji huo umeongezeka kutokana na miradi mikubwa iliyojengwa.

No comments:

Powered by Blogger.