TAIFA GAS YAPELEKA AJENDA YA MATUMIZI YA NISHATI SAFI MCHINGA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Meneja wa Taifa Gas kanda ya kusini, Hawa Juma akimkabidhi Makamu wa Rais Mheshimiwa Deogratius John Ndejembi moja ya mitungi iliyotolewa na kampuni kwa ajili ya kuwagawia wananchi, wakati wa ziara yake mkoani Lindi, wa pili kutoka kulia ni Mbunge wa jimbo la Mtama Mhe.Salma Kikwete ambaye alikuwa ni mwezeshaji wa zoezi hilo.
Makamu wa Rais Mheshimiwa Deogratius John Ndejembi akimkabidhi mtungi wa gesi mmoja wa wananchi.
***
Kampuni ya Taifa Gas inaendela kufanikisha ajenda ya matumizi ya nishati safi ambapo imegawa mitugi ya gesi 500 katika jimbo la Mchinga mkoani Lindi linaloongozwa na Mhe. Salma Kikwete.
Zoezi hilo limefanyika wakati wa ziara ya Makamu wa Rais, Mheshimiwa Deogratius John Ndejembi mkoani humo ambaye aligawa mitungi ya gesi kwa wananchi katika kijiji cha Kilangala na akasisitiza kuwa matumizi ya nishati yanasaidia kulinda afya za wananchi,kutunza mazingira na kupunguza gharama za maisha.
Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Salma Kikwete ambaye alikuwa ni mwezeshaji wa zoezi hilo aliwataka wananchi kutumia nishati safi ya kupikia ili kupunguza matumizi sambamba na kulinda afya zao.
Kampuni ya Taifa Gas imekuwa ikigawa mitungi ya gesi bure au kwa ruzuku katika sehemu mbalimbali nchini na kutoa elimu ya matumizi ya nishati safi ikiwa ni moja ya mkakati wake wa kuunga mkono ajenda ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuhamasisha utunzaji wa mazingira.





No comments: