LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAZIRI MKUU AKAGUA JENGO LA KISASA LA KITAALUMA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA KIZUMBI

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (katikati) akitembelea Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex) katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, wakati wa ziara yake mkoani Shinyanga, Novemba 9, 2026.  Picha na Kadama Malunde
Muonekano wa sehemu ya Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex) lililojengwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Shinyanga.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akisaini kitabu cha wageni katika moja ya ofisi zilizopo ndani ya Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex), katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Shinyanga.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akiwa katika moja ya madarasa ya kisasa yaliyopo ndani ya Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex), katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Shinyanga.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, akielezea kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex) lililojengwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex) lililojengwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Shinyanga.
Muonekano wa ndani wa moja ya madarasa ya kisasa yaliyopo katika Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex), lililojengwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Shinyanga.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akiondoka katika Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex) baada ya kukagua miundombinu ya kisasa ya kufundishia na kujifunzia katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Shinyanga, Novemba 9, 2026.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 Blog

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amesema Serikali itaendelea kuweka kipaumbele katika kuboresha mazingira ya kujifunzia katika taasisi za elimu ya juu nchini ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu katika mazingira bora yanayochochea maarifa, ubunifu na maendeleo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Jumatatu, Novemba 9, 2026, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya elimu ya juu katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, iliyopo mkoani Shinyanga.

Akiwa chuoni hapo, Waziri Mkuu ametembelea Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex), mojawapo ya majengo yaliyojengwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (Higher Education for Economic Transformation – HEET), unaolenga kuimarisha miundombinu na kuongeza ubora wa elimu ya juu nchini.
Akizungumza na wanafunzi na viongozi wa chuo hicho baada ya kukagua miundombinu hiyo, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuhakikisha mazingira ya kujifunzia yanaboreshwa, huku akiwataka wanafunzi kuweka jitihada katika masomo yao na kutumia fursa zilizopo kusonga mbele kielimu.

“Serikali itaendelea kuhakikisha inaweka kipaumbele kuhakikisha mazingira ya kujifunzia yanaboreshwa. Wekeni jitihada katika kujifunza, songeni mbele. Nawatakia kila la heri,” amesema Waziri Mkuu.

Akizungumzia ziara hiyo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema Waziri Mkuu amefika chuoni hapo kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi na kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi, na si kwa ajili ya kuzindua majengo hayo au kuweka jiwe la msingi.

“Tunashukuru sana Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amekuja kuangalia ujenzi umefikia wapi, hakuja kuzindua wala kuweka jiwe la msingi bali amekuja kuangalia na kukagua na kupata taarifa ya mradi, amepata pia muda wa kuzungumza na mkuu wa chuo na uongozi wa chuo. Tunamshukuru sana Waziri Mkuu,” amesema Prof. Mkenda.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda.

Ameeleza kuwa ujenzi wa miundombinu ya elimu ya juu unaotekelezwa katika mikoa mbalimbali nchini ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kusambaza fursa za elimu ya juu ili wananchi wengi zaidi waweze kupata huduma hiyo karibu na maeneo yao.

Akitolea mfano, amesema katika Kanda ya Ziwa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinajenga kampasi mkoani Kagera, huku Chuo Kikuu cha Ardhi na Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) zikiendelea na ujenzi wa kampasi zao Sengerema mkoani Mwanza.

Ameongeza kuwa mkoani Simiyu, Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM) inajenga kampasi yake, huku mkoani Mara Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere cha Kilimo na Teknolojia kikiwa kimeanza kupokea wanafunzi.

“Kwa hiyo tupo hapa Shinyanga ni mwendelezo wa shughuli hiyo, majengo mmeyaona, ujenzi unaendelea vizuri, hili ni jengo moja tumeliona lina madarasa na ofisi. Pia kuna hosteli ya wanafunzi wa kike,” amesema Prof. Mkenda.

Amesema ujenzi wa Jengo Mtambuka la Kitaaluma umegharimu Shilingi bilioni 5.5, akieleza kuwa fedha zilizotumika zimeleta matokeo yaliyokusudiwa kutokana na usimamizi mzuri wa uongozi wa chuo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, Mhe. Anne Makinda, ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amesema chuo hicho kina umuhimu wa kipekee kutokana na eneo kilipo ambalo shughuli za kilimo na ushirika ni sehemu muhimu ya maisha na uchumi wa wananchi.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, Mhe. Anne Makinda.

Amesema chuo hicho kina miundombinu ya kutosha ya kufundishia na kujifunzia inayoweza kuhudumia wanafunzi wengi, hata kufikia 2,000, huku akibainisha kuwa bado kuna uhitaji wa miundombinu ya malazi kwa wanafunzi wa kiume.

“Tunajivunia chuo hiki cha ushirika ambacho kimekaa katika sehemu ya wakulima na mambo ya ushirika ndiyo yanayofundishwa sana na mambo ya biashara, namna ya kuweka vitabu. Facilities za kufundishia zipo zote wanafunzi wengi wanatosha hata wangefika 2000. Mahali pa kulala ndiyo bado, wasichana ndiyo wamejengewa lakini wavulana bado halijaanza kabisa. Tunashukuru Serikali imesema itaendelea kusimamia ili haya majengo ya kujifunzia yasiwe peke yao,” amesema Makinda.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, Prof. Alfred Sife, amesema mradi wa HEET umewezesha ujenzi wa majengo mawili makubwa katika taasisi hiyo ambayo ni Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex) na hosteli ya wanafunzi wa kike.
Amesema majengo hayo yamekamilika na kuanza kutumika rasmi katika muhula wa pili wa mwaka wa masomo 2025/2026, hatua iliyoongeza uwezo wa chuo kuhudumia wanafunzi wengi zaidi na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

Ameeleza kuwa Jengo Mtambuka la Kitaaluma lina ghorofa mbili na ukubwa wa mita za mraba 3,800, likiwa na miundombinu ya kisasa inayojumuisha madarasa, kumbi mbili za mihadhara zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 600, vyumba vinne vya mihadhara vyenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 400 kwa wakati mmoja na vyumba vitatu vya semina vinavyoweza kuchukua watu 150.
Aidha, jengo hilo lina ofisi 13 za watumishi, kituo cha kukuza ubunifu wa biashara, maabara ya kompyuta yenye uwezo wa kuhudumia watumiaji 40 kwa wakati mmoja pamoja na chumba cha kunyonyeshea watoto.

Kwa upande wa hosteli ya wanafunzi wa kike, amesema jengo hilo lina ghorofa moja na vyumba 55 vyenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 212. Pia lina ofisi ya mlezi wa wanafunzi, chumba cha huduma ya kwanza, sehemu ya kupumzikia (lounge), chumba cha kompyuta, sehemu za kufulia na kuanikia nguo, vyoo 22, mabafu 19 na stoo mbili.
Kuhusu gharama za utekelezaji, Prof. Sife amesema ujenzi wa majengo hayo mawili umegharimu jumla ya Shilingi 8,976,348,732.36, huku kiasi cha Shilingi 435,989,255 kikiwa kimebaki kama fedha za dhamana ya matengenezo (Retention Money), zinazotarajiwa kulipwa baada ya kukamilika kwa kipindi cha dhamana tarehe 13 Machi 2027.

Hata hivyo, amesema mradi huo bado una mahitaji ya ziada yanayohitaji kushughulikiwa ili kukamilisha baadhi ya kazi na kuimarisha matumizi ya miundombinu iliyojengwa.

Amezitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ongezeko la gharama za vifaa na huduma za ujenzi kutokana na mabadiliko ya bei (Price Variations), ambapo fedha zinazohitajika kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa hosteli ya wanafunzi wa kike zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani 1,243,366.62.

Changamoto nyingine ni kuahirishwa kwa ujenzi wa hosteli ya wanafunzi wa kiume uliokuwamo katika mpango wa awali wa mradi kutokana na sababu za kibajeti, pamoja na kutokuwepo kwa jengo la utawala ambalo ujenzi wake unakadiriwa kugharimu Dola za Marekani 3,304,687.88.

Kutokana na mahitaji hayo, Prof. Sife amesema uongozi wa chuo unaomba Serikali kuendelea kuwezesha upatikanaji wa fedha ili kukamilisha miundombinu hiyo na kuhakikisha wanafunzi wanapata huduma muhimu za malazi na utawala katika mazingira bora.

Mradi wa HEET ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuimarisha elimu ya juu nchini kupitia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu, kuongeza ubora wa mafunzo, kuimarisha utafiti na ubunifu pamoja na kuoanisha elimu inayotolewa na mahitaji ya soko la ajira.
Wanafunzi wa Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB) wameishukuru Serikali kwa uwekezaji uliofanyika kupitia mradi wa HEET, wakisema maboresho ya miundombinu ya chuo hicho yameongeza ubora wa mazingira ya kufundishia na kujifunzia, kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu za kitaaluma na kuwapa motisha zaidi katika masomo yao.

ANGALIA MATUKIO KATIKA PICHA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akizungumza akiwa ndani ya moja ya madarasa ya kisasa katika Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex), Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), mkoani Shinyanga, Novemba 9, 2026.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akiwa amekaa na viongozi mbalimbali ndani ya moja ya madarasa ya kisasa katika Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex), Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), mkoani Shinyanga, Novemba 9, 2026.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akiwa amekaa na viongozi mbalimbali ndani ya moja ya madarasa ya kisasa katika Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex), Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), mkoani Shinyanga, Novemba 9, 2026.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, akielezea kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, Mhe. Anne Makinda, akizungumzia utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya kisasa ya kufundishia na kujifunzia katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, mkoani Shinyanga, Novemba 9, 2026.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akipokea maelezo kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, Prof. Alfred Sife, kuhusu ujenzi wa Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex), Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), mkoani Shinyanga, Novemba 9, 2026.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akizungumza na wanafunzi wa Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya elimu ya juu mkoani Shinyanga.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akizungumza na wanafunzi wa Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya elimu ya juu mkoani Shinyanga.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akiondoka katika Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex) baada ya kukagua miundombinu ya kisasa ya kufundishia na kujifunzia katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Shinyanga, Novemba 9, 2026.
Muonekano wa sehemu ya Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex) lililojengwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex) lililojengwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex) lililojengwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex) lililojengwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex) lililojengwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex) lililojengwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Shinyanga.
Muonekano wa ndani wa moja ya madarasa ya kisasa yaliyopo katika Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex), lililojengwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Shinyanga.
Muonekano wa ndani wa moja ya madarasa ya kisasa yaliyopo katika Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex), lililojengwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Shinyanga.
Muonekano wa ndani wa moja ya madarasa ya kisasa yaliyopo katika Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex), lililojengwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Shinyanga.
Muonekano wa ndani wa moja ya ukumbi mdogo katika Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex), lililojengwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex) lililojengwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Shinyanga.
Muonekano wa ndani wa moja ya ukumbi mkubwa ambao bado haujawekewa samani katika Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex), lililojengwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex) lililojengwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex) lililojengwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya Jengo Mtambuka la Kitaaluma (Academic Complex) lililojengwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Shinyanga.

No comments:

Powered by Blogger.