BENKI YA CRDB YAKABIDHI VITI, MEZA BARIADI MKOANI SIMIYU
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Benki ya CRDB imetoa msaada wa madawati 80 (viti na meza) katika shule ya msingi Giriku B pamoja na shule ya sekondari Ikungulyambeshi zilizopo katika Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.
Akikabidhi madawati hayo Novemba 03, 2026 kwa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Simon Simalenga, Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Ziwa Denis Mwoleka alisema hatua hiyo inalenga kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga aliipongeza benki ya CRDB kwa kurejesha kwa jamii sehemu ya faida yake na hivyo kuwahimiza wananchi kuendelea kutumia huduma za benki hiyo katika shughuli zao za kiuchumi ili iendelea kuwasaidia katika sekta mbalimbali za maendeleo.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Ikungulyambeshi, Minza Maduhu aliishukuru benki ya CRDB Kwa msaada wa madawati 40 kwa kila shule na kwamba hatua hiyo itapunguza changamoto ya upungufu wa madawati kwa wanafunzi.
Meneja wa benki ya CRDB Kanda ya Ziwa- Denis Mwoleka (kushoto), akikabidhi madawati kwa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu- Simon Simalenga (kulia) kwa ajili ya shule ya msingi Giriku B pamoja na shule ya sekondari Ikungulyambeshi.








No comments: