LIVE STREAM ADS

Header Ads

PSSSF YAENDESHA SEMINA KWA MAAFISA UTUMISHI MKOANI MARA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeendesha semina kwa Maafisa Utumishi Mkoa wa Mara, ili kuwajengea uelewa wa kushughulikia kwa weledi masuala ya wanachama wa mfuko huo.

Semina hiyo imefanyika Ijumaa Novemba 06, 2026 katika Wilaya ya Musoma mkoani Mara ambapo washiriki wa semina hiyo wamehimizwa kuwasaidia wanachama wa PSSSF kupata huduma bora na kwa wakati.

Akifungua semina hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mara Brigedia Jenerali Evans Mtambi amesema semina hiyo ikasaidie kuongeza ufanisi katika upatikanaji wa huduma za PSSSF hususani matumizi ya huduma za kidigitali kwa wanachama.

“Zamani mtu alikuwa anafunga safari kwenda Dar es salaam, Dodoma au makao makuu ya mkoa, lakini sasa hivi anawasha tu bando kwenye simu yake, anawasilisha hitaji lake na anahudumiwa akiwa nyumbani” amesema RC Mtambi.

Naye Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa, CPA. Rajabu Kinande amesema ili kuhakikisha mfuko huo unatoa huduma bora na ya haraka, umejikita kuwafikia wanachama wake kwa njia ya kidigitali.

“Sasa hivi mteja anaweza kupata huduma kupitia simu yake ya mkononi hivyo ili kuhakikisha huduma hiyo inaenda vizuri tukaona ni vyema kukutana na maafisa utumishi ambao wana wajibu wa kutusaidia kutoa huduma bora kwa wanachama” amesema CPA. Kinande.

Akitoa shukurani kwa niaba ya Maafisa Utumishi mkoani Mara, Jumanne Obogo ambaye ni Afisa Utumishi Halmashauri ya Musoma Vijijini amesema semina hiyo itawasaidia kuwahudumia kwa ufanisi watumishi kupitia mfumo wa kidigitali.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Brigedia Jenerali Evans Mtambi akizungumza kwenye ufunguzi wa semina kwa Maafisa Utumishi mkoani humo, iliyoandaliwa na Mfuko wa PSSSF.
Maafisa Utumishi mkoani Mara wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mara Brigedia Jenerali Evans Mtambi.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Juma Chikoka akitoa salamu kwenye semina hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Juma Chikoka akitoa salamu kwenye semina kwa Maafisa Utumishi mkoani Mara.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa, CPA. Rajabu Kinande akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Meneja wa PSSSF Mkoa wa Mara akitoa salamu kwenye semina hiyo.
Maafisa Utumishi mkoani Mara na Watumishi wa PSSSF wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mara Brigedia Jenerali Evans Mtambi.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI

No comments:

Powered by Blogger.