PSSSF YATOA ELIMU YA FEDHA KWA WASTAAFU MWANZA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com .
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umetoa mafunzo maalumu kwa wastaafu wa utumishi wa umma mkoani Mwanza, ili kuwajengea uelewa kuhusu huduma zinazotolewa na mfuko huo pamoja na elimu ya fedha.
Akifungua mafunzo hayo Ijumaa Oktoba 30, 2026, Katibu Tawala Msaidizi Taaluma mkoani Mwanza, Mwl. Martin Nkwabi, aliwahimiza wastaafu na wanaojiandaa kustaafu kutambua kwamba kustaafu ni mwanzo wa hatua nyingine ya maisha na si mwisho wa maisha yao.
Nkwabi alisema mafunzo hayo yatawasaidia wastaafu kujiandaa kiuchumi, kuwakinga dhidi ya umaskini na kuwaelimisha namna ya kujiepusha na vitendo vya udanganyifu baada ya kulipwa mafao yao
Naye Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa, Rajab Kinande, aliwashauri watumishi wa umma kuanza maandalizi ya kustaafu mapema na kuwa makini na matapeli wanaotumia mbinu mbalimbali kuwatapeli mafao yao baada ya kustaafu.
Kinande alisema mfuko huo umeanzisha kaulimbiu mpya isemayo "PSSSF Leo na Kesho Pamoja", inayolenga kutoa elimu na huduma kwa wanachama katika kipindi chote cha utumishi wao badala ya kusubiri wanapokaribia kustaafu au kustaafu.
Akizungumza kwa niaba ya wastaafu, Subira Elfasi aliipongeza PSSSF kwa kuendelea kuboresha huduma kwa wastaafu, ikiwemo mafunzo ya elimu ya fedha ambayo yanawasaidia kujikwamua kiuchumi baada ya utumishi wa umma.
Katibu Tawala Msaidizi Elimu Mkoa wa Mwanza, Martin Nkwabi.
Wastaafu wakifuatilia ufunguzi wa mafunzo hayo.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa, Rajab Kinande.
Wastaafu wakifuatilia mafunzo hayo.
Wastaafu jijini Mwanza.
No comments: